Godbless Lema Aliamsha Dude Bungeni, Hali ya Hewa Yatibuka

by: Global TV Online     Published on: 03 July 2017

Views: 298,997

1,105    180   

Fast Download

Description :

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amechafua hali ya hewa bungeni akipinga muswada wa mabadiliko ya sheria ya maliasili, wakati akichangia hoja huku akiwatuhumu wabunge wa CCM kufanya mambo kwa ushabiki.Lema amesema sheria zilizoligharimu taifa mpaka sasa, zilipitishwa kishabiki bungeni, kama ambavyo wabunge wanataka kufanya hivyo sasa hivyo kama ushabiki utaendelea, lazima sheria zitakazopitishwa zitakuwa ni zilezile.Ilibidi mheshimiwa George Simbachawene, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, asimame na kumkosoa Lema kwamba alikuwa akikiuka sheria katika uchangiaji wake lakini alipokaa, Lema alimpiga kijembe kwamba anataka kubadilishiwa wizara ndiyo maana anapinga hoja ya Lema. Akataka utengwe muda wa kutosha kujadili muswada huo na si kupeleka bungeni kwa hati ya dharura. Mjadala mkali uliendelea ambapo Lema aliendelea kutoa hoja nzito akizielekeza upande wa wabunge wa CCM.